Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, mashindano ya kitaifa ya Qur’ani ya Brunei yanayofanyika mwezi Aprili yana washiriki 12 katika hatua ya nusu fainali. Hatua hiyo inawajumuisha wasomaji wa Qur’ani wanaume waliopata alama zaidi ya 85, na wasomaji wanawake waliopata alama zaidi ya 80 (kutokana na idadi ndogo ya washiriki wanawake) katika makundi ya wanaume na wanawake.
Warsha hii inatoa fursa kwa wasomaji wa Qur’ani wa nchi hiyo kupata mafunzo ya ana kwa ana kutoka kwa wakufunzi wenye uzoefu na ustadi katika fani ya usomaji wa Qur’ani.
Washiriki pia wanapata nafasi ya kuongeza maarifa yao kupitia warsha ya Taranum, kufanya tafiti za Qur’ani, pamoja na kujifunza maana na tafsiri zake.
Warsha hii ya siku tano inafanyika katika Ukumbi wa Multaqa ndani ya Wizara ya Ulinzi ya Brunei.
Chanzo: Borneo Bulletin
Maoni yako